Sunday, February 13, 2011

YANGA PWAA..SIMBA KUJIULIZA KWA WACOMORO LEO



 Wababe wa Yanga DEDEBIT FC

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho timu ya soka ya YANGA imeyaaga mashindano hayo rasmi baada ya kukubali kichapo cha mqabao 2-0 kutoka kwa DEDEBIT FC ya Ethiopia.

Kwa matokea hayo YANGA imeyaaga mashindano hayo kwa jumla ya mabao 6-4 Baada ya timu hizo kwenda sare ya 4-4 katika mchezo uliofanyika wiki mbili zilizopita katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam

Wakati YANGA yakiwakuta hayo Wapinzani wao wakuu hapa nchini wawakilishi katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika Timu ya SIMBA leo watashuka katika dimba la uhuru kulipiziana kisasi na mabingwa wa Comoro FC ELAN

Mchezo huo unatazamiwa kuwa wa vuta ni kuvute kutokana n kila timu kuhitaji ushindi ili iweze kusonga mbele baada ya kutoka suluhu tasa katika mchezo wa awali uliofanyika wik,i mbili zilizopita nchini COMORO


Kkosi cha simba kitakachowavaa Wacomoro leo.