Wednesday, January 26, 2011

FALLY IPUPA AMPORA MCHUMBA ESSIEN

 Anaitwa Nadia Buari a.k.a BEYONCE

 Mwanamuziki maarufu wa DRC Fally ipupa amezua minong'ono midompni mwa watu wengi baada ya kuonekana akitanua sehemu mbalimbali na aliyekuwa mchumba wa mwanasoka wa ghana na klabu ya Chelsea Michael Essien, Nadia buari

Fally alionekana kwa mara ya kwanza akiwa na Nadia wakati wa tuzo za MAMA nchini Nigeria ambapo baada ya hafla ya utoaji yuzo hizo wawili hao walionekana wakiondoka pamoja mpaka kwenye hoteli aliyofikia Fally ipupu na inadaiwa walilala hapo pamoja.

Lakini weekend iliyopita wawili hao wameonekana pamoja wakitanua jijini Johansburg Africa kusini ambapo Fally yupo huko kwa ajili ya shoo maalum hali inayosemekana wamekolea katika penzi zito.

Nadia Buari mtoto wa mwanamuziki wa zamani wa ghana Alhaji Sidiku Buari inasemekana ametengana na mpenzi wake wa siku nyingi Michael Essien kwa sasa ni moja ya waigizaji nyota wenye mvuto nchini ghana ambapo anakumbwa na kashfa za kubadili wapenzi mara kwa mara

Miongoni mwa filamu zilizomtoa mrembo huyo ni pamoja na Darkness of sorrow,Mummy Daughter,na Beyonce the president Daughter.


 Nadia akiwa na Fally


 Hapa akiwa na Essien


 Hapa akiwa na Van Vicker


 Nadia Buari kwenye pozi