Saturday, March 12, 2011

VIJANA WA MJENGONI WALIPOAMUA KUPUMZISHA AKILI WEEKEND HII



 MTOTO SHADEE
 MULI B
 ONE LOVE muli,Anord,Shadee,B12 na Mirad Ayo



 Anold Kayanda na Muli B

 Dina Marious yeye aliamua kuwa mtazamaji

UEOAJI TUZO WA DADA BORA WA NYUMBANI ULIVYOFANA MJENGONI


 Mtangazaji wa kipindi cha Leo tena Dina Marious akiwa na Zamaradi Mketema




 Mahojiano ndani ya studio namba mbili

NI VITA LEO MAN UNITED VS ARSENAL

Dakika 90 kuamua nani mbabe?

 Manchester United na Arseanal zinakutana eo katika dimba la OLD TRAFFORD katika robo fainali ya kombe la FA huku kila timuikwa na maumivu makali baada ya kuboronga katika michezo yao iliyopita.

Wakati man u wakiugulia vipigo viwili mfululizo toka kwa chelsea na Liverpool wao Arsenal bado wanaweweeka na kupokwa ubingwa wa CARLING na Birminingham pamoja na kutolewa katika michuano ya UEFA na Barcelona.

Hali hiyo ndiyo inayofanya mchezo wa leo kutotabilika na mwamuzi pekee ni dk 90 tu ndipo tutajua nani anaendelea na maumivu na nani amepunguza maumivu.

Wednesday, March 9, 2011

ARSENAL YAFIA NOU CAMP


 Barcolona jana walidhihirisha ubabe wao baada ya kuwatoa nishai Arsenal kwa kuichapa mabao 3-1 katika mchezo wa ligi ya mabingwa ulaya uliofanyika katika dimba la NOU CAMP nchini Hispania

Shujaa wa mchezo huo ni mchezaji bora wa duni Leonel M ssi aliyefunga mawili huku Xavi akifunga moja


Kadi ya utata


Xavi


Messsssssssssiiii


kama anamwambia"pole mdogo wangu"





Monday, March 7, 2011

NI VITA UEFA CHAMPIUONS LEAGUE


Kindumbwendumbwe cha ligi ya mabingwa barani ulaya kinatarajiwa kuendelea tena kesha kwa Arsenal kupambana na Barcelona huku Tottenham wakiwaarika majeruhi AC MILAN katika dimba la Acton Pack

Mechi ya Arsenal na Barcelona ndiyo iliyoonekana kukamata vichwa vya wengi mara baada ya Arsenal kuiangamiza Barca 2-1 katika mchezo wa awali uliofanyika katika dimba la EMIRATES nchini Uingeleza

Sunday, February 27, 2011

BONGO FLEVA WAWAPELEKA PUTA WACHEZA FILAMU

Ally kiba shujaa wa mchezo

 Kikosi ca Bongo Fleva
Kikosi cha wana muziki wa kizazi kipya jana kilidhihirisha ubabe wake kwa wenzao waigizaji muvi baada ya kuwatandika 2-0 katika mchezo maalum ulioandaliwa na CLOUDS FM na CLOUDS TV kwa ajili ya kuchangia waathirika wa mabomu yaliyolipuka gongo la mboto

Shujaa wa Bongo fleva katika mchezo huo ni mwanamuziki H BABA aliyetupia goli zote wavuni baada ya kumalizia kazi nzuri zilikuwa zikifanywa na Ally Kiba
 'Wazee wa location' Kikosi cha Bongo Movie


 Shabiki kwa raha zake



 Ahsanteni Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi
THT DANCES walikuwepo kutoa burudani

Mavituuuuz ya Ally Kiba

 Adam Mchomvu kutoka mjengoni


Hatimaye wana BONGO FLEVA wakajitwalia mwali wao

Hapa dogo janjaro hapa Diamond ni raha tuuuu

Wednesday, February 23, 2011

KINDUMBWENDUMBWE UEFA LEO


Michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya inatarajiwa kuendelea tena leo wakati mashetani wekundu (man united ) wakiwa wageni wa Olympic marseille huku AC MILAN wakiwaalika BAYERN MUNICH.
Hapo jana CHELSEA walikandamiza FC COPPENHAGEN mabao 2-1 huku MADRID wakienda sare ya 1-1 na LYON.

WA BONGO FLEVA, FILAMU DIMBANI J MOSI

Vikosi vya wachezaji wa timu ya waimba muziki wa kizazi kipya na waigiza filamu Tanzania
 vinatarajia kupambana jumamaosi hii katika dimbA la Taifa kuchangisha pesa kwa ajili ya wahanga wa mabomu ya GONGO LA MBOTO

Maandalizi kwa ajili ya mpambano huo yamekamilika na kinachosubiliwa ni siku husika huku kila timu ikijinoa vilivyo kwa mtanange huo

Wadau tunapaswa kujitokwza kwa wingi kuwachangia ndugu zetu wa GONGO LA MBOTO

Thursday, February 17, 2011

BREKING NEEEEEEWS

HALI BADO SI SHWALI GONGO LA MBOTO

 Kama sio Tanzania vile lakini hiyo ndio hali halisi
 

 Ambulance zilipiga trip kwa sana



 Ni kuchapa mbio tu usiku wa jana hali ni tete sana



 Majeruhi akipata huduma ya kwamza




 Daktari wa Hospitali ya amana akiwa amembeba mtoto aliyepoteza wazazi wake
 


 Askari akisaidia majeruhi wa mabomu ya Gongo la mboto




 Meya wa jiji la Dar es Salaam Jerry Silaa akiwa katika tukio hilo jana usiku


Sunday, February 13, 2011

HAPPY VALENTINE DAY WADAU




KESHO watanzania kote nchini wanaungana na watu wote DUNIANI kuadhimisha SIKU YA WAPENDANAO maarufu kama 'VALENTINE DAY' ambayo kidunia huadhimishwa kila ifikapo tarehe 14 februari.

Ni matumaini yangu kuwa tutaadhimisha siku hii kwa amani na Upendo kwa kuzingatia maadili ya KITANZANIA

 H aya jamani

YANGA PWAA..SIMBA KUJIULIZA KWA WACOMORO LEO



 Wababe wa Yanga DEDEBIT FC

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la shirikisho timu ya soka ya YANGA imeyaaga mashindano hayo rasmi baada ya kukubali kichapo cha mqabao 2-0 kutoka kwa DEDEBIT FC ya Ethiopia.

Kwa matokea hayo YANGA imeyaaga mashindano hayo kwa jumla ya mabao 6-4 Baada ya timu hizo kwenda sare ya 4-4 katika mchezo uliofanyika wiki mbili zilizopita katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam

Wakati YANGA yakiwakuta hayo Wapinzani wao wakuu hapa nchini wawakilishi katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika Timu ya SIMBA leo watashuka katika dimba la uhuru kulipiziana kisasi na mabingwa wa Comoro FC ELAN

Mchezo huo unatazamiwa kuwa wa vuta ni kuvute kutokana n kila timu kuhitaji ushindi ili iweze kusonga mbele baada ya kutoka suluhu tasa katika mchezo wa awali uliofanyika wik,i mbili zilizopita nchini COMORO


Kkosi cha simba kitakachowavaa Wacomoro leo.

BAO LA MWAKA..UNABISHAAAA....?

 Wayne Ronney akifunga kwa tik-tak jana dhidi ya mahasimu wao Man City

Mshambuliaji Wayne Rooney jana aliwalaza vema wapenzi wa Man United baada ya kuifungia timu yake bao mwanana ambalo linasemekana halijawahi kufungwa tangu kuanza kwa msimu huu.

Rooney alipiga bao hilo akiipa Man U ushindi wa 2-1 dhidi ya mahasimu wao Manchester City mchezo uliosukumwa katika dimba la Old Trafford.


Wayne Rooney akishangilia na Luis Nani jana





Wednesday, February 9, 2011

STARS KULIPUANA NA WAPALESTINA TAIFA LEO.

 Kikosi cha 'STARS'

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo wanaingia dimbani katika dimba jipya la Taifa kukabiliana na 'vibonde'Timu ya Taifa ya Palestina katika mchezo maalum wa kirafiki uliopo katika kalenda inayotambuliwa na shirikisho la soka duniani FIFA

Stars inaingia uwanjani jioni ya leo pasipo nyota wake kadhaa kutoka kwenye  timu za YANGA na MTIBWA SUGAR ambazo zilikuwa nje ya DAR ES SALAAM kwenye michuano ya ligi kuu Tanzania Bara mwishoni mwa wiki.

Kwa mujibu wa Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Boniface Wambura maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yamekwisha kamilika na kinachosubiliwa ni muda mwafaka wa mtifuano huo.

MFALME WA RHYMES AMEPATWA NA NINI?

 'SIMBA DUME'Mfalme SULEIMAN MSINDI a.k.aAfande Selle

Ni kama miujiza hivi but ukweli unabaki kuwa palepale kuwa huyu ndio mwenye kofia ya UFALME WA RHYMES Tanzania mpaka sasa hivi majuzi alijikuta akisaula jukwaani bila aibu,sasa sijui ndio tuseme ni swagga za 2011 au ndio swagga za mfalme a.k.a SIMBA DUME....Tarfakari kisha chukua hatua mwenyeweeeeeeeeeeeeee against huyu MFALME

UNIVERSITY CORNER IS BACK


"Kila mmoja anapendezaa..hakuna inayomchukizaa.. sitoweza kuiacha inanitoa chicha nami ninawakilishaaa.."
"Sasa ni burudani ndani ya Tshirt na jeans hata ikiwa mpauko ili mradi iwwakilishe jeans..jeans ni jeans iwe suruali au pensi ikinata na mwili lazima uipe nafasi ingia club kisha fanya research ya mavazi wengi utawaona wamevaa Tshirt na jeans"

Si unaikumbuka hii ngoma jinsi ambavyo ilibamba miaka ya 2002-2003 na si unawakumbuka hawa jamaa walioripua mzigo huu?

Jamaa wanaitwa UNIVERSITY CORNER kundi lililokuwa likiundwa na na vichwa viwili DIRA na TASWIRA basi jamaa wapo mbioni kurudi februari hii na tayari wamejipanga kuja kufanya uvamivi wa ajabu ndani ya tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Wakizungumza na blog hii jamaa hao waliotesa na ngoma kama T HIRT NA JEANS na ile ya VUMILIA wamesema wapo tayari kwa changamoto iliyopo na wanatamani sana kufanya kazi na maproducer watatu ambao ni LAMAA, DUKE  na HAMMIE B

Tuesday, February 8, 2011

MAANDALIZI UZINDUZI WA ALBUM YA CPWAA YAKAMILIKA

Mkali wa style ya cranker Tanzania CPWAA amekamilisha maandalizi ya uzinduzi wa album yake atakayoizindua siku ya jumapili ndani NEW MAISHA CLUB huku akipewa tafu na mchizi wake wa siku nyingi SUMA LEE ambae aliunda nae kundi la PARKLANE.

Akizungumzia uzinduzi huo alipokuwa akifanya mahojiano na blog hii mtu mzima CPWAA amesema kuwa kila kitu kiko fresh na kinachosubiliwa ni siku husika tu ili aweze kudhihirisha kuwa kwa nini anaitwa ''CRANK MASTERS''

''Nimejipanga kufanya uzinduzi babkubwa na wa kihistoria jumapili ndani ya NEW MAISHA CLUB nadhani utakuwa ni uzinduzi wa kwanza kwa hapa bongo kufanyika ninachowaomba fans wangu wajitokeze kwa wingi kushuhudia makamuzi ya ukweli''alitanabaisha CPWAA