Wednesday, February 9, 2011

UNIVERSITY CORNER IS BACK


"Kila mmoja anapendezaa..hakuna inayomchukizaa.. sitoweza kuiacha inanitoa chicha nami ninawakilishaaa.."
"Sasa ni burudani ndani ya Tshirt na jeans hata ikiwa mpauko ili mradi iwwakilishe jeans..jeans ni jeans iwe suruali au pensi ikinata na mwili lazima uipe nafasi ingia club kisha fanya research ya mavazi wengi utawaona wamevaa Tshirt na jeans"

Si unaikumbuka hii ngoma jinsi ambavyo ilibamba miaka ya 2002-2003 na si unawakumbuka hawa jamaa walioripua mzigo huu?

Jamaa wanaitwa UNIVERSITY CORNER kundi lililokuwa likiundwa na na vichwa viwili DIRA na TASWIRA basi jamaa wapo mbioni kurudi februari hii na tayari wamejipanga kuja kufanya uvamivi wa ajabu ndani ya tasnia ya muziki wa kizazi kipya.

Wakizungumza na blog hii jamaa hao waliotesa na ngoma kama T HIRT NA JEANS na ile ya VUMILIA wamesema wapo tayari kwa changamoto iliyopo na wanatamani sana kufanya kazi na maproducer watatu ambao ni LAMAA, DUKE  na HAMMIE B