Tuesday, February 8, 2011

MAANDALIZI UZINDUZI WA ALBUM YA CPWAA YAKAMILIKA

Mkali wa style ya cranker Tanzania CPWAA amekamilisha maandalizi ya uzinduzi wa album yake atakayoizindua siku ya jumapili ndani NEW MAISHA CLUB huku akipewa tafu na mchizi wake wa siku nyingi SUMA LEE ambae aliunda nae kundi la PARKLANE.

Akizungumzia uzinduzi huo alipokuwa akifanya mahojiano na blog hii mtu mzima CPWAA amesema kuwa kila kitu kiko fresh na kinachosubiliwa ni siku husika tu ili aweze kudhihirisha kuwa kwa nini anaitwa ''CRANK MASTERS''

''Nimejipanga kufanya uzinduzi babkubwa na wa kihistoria jumapili ndani ya NEW MAISHA CLUB nadhani utakuwa ni uzinduzi wa kwanza kwa hapa bongo kufanyika ninachowaomba fans wangu wajitokeze kwa wingi kushuhudia makamuzi ya ukweli''alitanabaisha CPWAA