Wednesday, February 2, 2011

MAN U, ARSENAL, CHELSEA ZANG'ARA ENGLAND

 Wayne Rooney akishangilia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya Aston Villa jana.
Manchester United imezidi kujikita kileleni mwa ligi kuu ya soka nchini uingereza baada ya jana kuifunga Asto Villa 3-1 katika dimba la Old Trafford.

Wayne Rooney alizinduka toka kwenye usingizi mzito na kutupia mbili nyavuni kabla ya Luis Nani kokandamiza la tatu na kuihakikishia man u ushindi mnono wa na pointi tano juu ya wanaowafuata Arsenal.

Katika mechi nyingine za hapo jana Arsenal iliwanyanyasa Everton kwa kuishindilia mabao 2-1 huku Chelsea ikiwa na Fernando Torres wakiichabanga bila huruma Sunderland 4-2.



 Daren Clichy akichuana na Coullen wa Evarton jana.



 Frank Lampard akiifungia CHELSEA bao la pili dhidi ya Sunderland jana.