Saturday, January 22, 2011

YANGA YAIFANYIA MAUAJI AFC

 Kikosi cha Yanga

Timu ya soka ya Yanga ys jijini Dar es Salaam jana waliianza vizuri ngwe ya pili ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara maarufu kama Vodacom premier league baada ya kuichabanga bila huruma timu ya AFC ya Arusha mabao 6-1 mchezo uliofanyika kwenye dimba la uhuru.

Mashujaa wa yanga katika mtanange huo walikuwa ni Davis Mwape aliyetupia matatu wavuni,Iddi mbaga alifuga mawili pamoja na Shedrack Nsajigwa aliyefunga bao moja.

Bao pekee la AFC liliwekwa kimiani na Bakari Kigodeko katika dakika ya 66 na kwa matokeo hayo yanga imeshika usukani wa ligi kuu kwa kufikisha jumla ya pointi 28 bbada ya kushuka dimbani mara 12 wakiwaacha watani wao wa jadi Simba katika nafasi ya pili kwa kua na pointi 27