Sunday, January 23, 2011

SIMBA HOI KWA WAUZA ICE CREAM 'AZAM'


Ligi kuu ya soka Tanzania Bara imeendelea tena jioni ya leo kwa kushuhudiwa mchezo mmoja ukipigwa kwenye dimba la Uhuru(Shamba la bibi) ambapo wekundu wa msimbazi simba walikuwa wakiparuana na wauza ice cream wa Azam FC  na katika mchezo huo Simba wamekubali kichapo cha mabao 3-2.

Mwiba mkali katika mchezo huo kwa upande wa Simba alikuwa ni mshambuliaji Mrisho ngassa aliyeisumbua sana safu ya ulinzi ya wekundu hao wa msimbazi akisaidiwa na mshambuliaji mrefu John Boko(Adebayo)

Mabao ya AZAM katika mchezo huo yalitupiwa kimiani Ngassa pamoja na John Boko  huku yale ya simba yakifungwa na Nicco Nyagawa na Hillary Echessa.


Kwa matokeo hayo Simba imeendelea kubaki na pointi zake 27 huku azam wakijiongezea pointi na sasa wametimiza pointi 23.ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena kesho kwa watoto wa jangwani yanga kucheza na polisi Dodoma kwenye uwanja wa uhuru.
 Kocha Mkuu wa Simba Patrick Phiri akitoa maelekezo kwa wachezaji wake.
 Kikosi cha SIMBA

 Patashika langoni