Wednesday, January 19, 2011

SIMBA ATLETICO FREE KESHO

Mabingwa wa Tanzania Simba kesho wanatarajia kutupa karata yao kwenye dimba la Taifa kwa kupepetana na Atletico ya brazil.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa timu hiyo ya brazili baada ya hapo jana kuiangamiza yanga mabao 3-1.

Kwa mujibu wa kocha mkuu wa simba mzambia patrick phili amenukuliwa akisema atautumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yao muhimu ya kujiandaa na ligi kuu pamoja na michuano ya klabu bingwa afrika.

Mchezo huo umetangazwa kutokua na viingilio baada ya jana kutokuwa na watu wengi uwanjani hivyo uongozi wa simba umewataka wapenzi na wanachama wake kujitokeza kwa wingi kesho.
 Kikosi cha simba na viongozi wao katika picha ya pamoja