Tuesday, January 25, 2011

HIS NAME IS 'DAVIS MWAPE' ANATISHAAA.....

 Mtambo mpya wa mabao jangwani 'Davis Mwape'
Nyota njema imeendelea kumwakia mshambuliaji mpya wa Yanga Davis Mwape katika ligi kuu ya vodacom baada ya jana kupachika mabao mawili muhimu yaliyoipatia klabu yake pointi tatu muhimu dhidi ya timu ya Polisi Tanzania mchezo uliochezwa kwenye dimba la uhuru jijini Dar es Salaam.

Mabao hayo ya mwape yanakuja siku mbili tu baada ya kufunga mabao mengine matatu dhidi ya AFC ya Arusha katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya ligi siku ya ijumaa ya wiki iliyopita ambapo yanga ilishinda mabao 6-1

Mpaka sasa Mwape ana jumla ya mabao matano katika mechi mbili alizocheza hali anayomfanya kumuweka katika kiwango bora zaidi cha kufanya vizuri katika ligi kuu inayoendelea na kuwaweka matumbo joto waliomtamngulia katika ufungaji.