Tuesday, January 25, 2011

DOGO JANJA NDANI YA SKULI

 Dogo janja ndani ya Unifomu.
Rapper mahili anayechipukia kutoka kundi la TIPTOP CONNECTION 'Dogo janja'amesema kuwa kwa sasa anakaza buti zaidi kwenye book kwani anataka kuwaonyesha washabiki wake kuwa yeye ni mkali sio kwenye kuchana tu bali hata kwenye mambo ya kielimu ambapo amesema kuwa elimu kwake ndio kitu cha msingi zaidi ya mambo yote.

Dogo janja ambaye sasa anatamba na ngoma yake mpya ya 'mtoto wa uswazi' aliyomshirikisha mkali toka salasala 'Godzilla' amesema kuwa atahakikisha matokeo ya midterm hii yanakua mazuri zaidi ili kuwatoa wasiwasi wazazi wake.

"Unajua kwa sasa nataka kupiga book mpaka nifanye vizuri ili wazazi wasiwe na wasiwasi kuwa muziki utanirudisha nyuma kielimu"alisema Dogo Janja.

Dogo janja anasema anaushukuru sana uongozi na wanafunzi wenzake wote wa Makongo High School kwa sababu wamempokea vizuri na anashirikiana nao vizuri katika masuala ya elimu.


 DOGO JANJARO.