Wednesday, January 26, 2011

HAWA NDIO WAPINZANI WA YANGA KOMBE LA SHIRIKISHO

 KIKOSI CHA DEDEBIT
Kikosi kamili cha timu ya DEDEBIT Kinatarajia kuwasili nchini usiku wa leo tayari kwa mpambano wao dhidi ya Yanga unaotarajia kufanyika siku ya jumamosi katika dimba la Taifa huku kikiwa ma matumaini makubwa ya kuibuka na ushindi katika mechi hiyo

Tayari uongozi wa Yanga umeshatangaza viingilio vya mechi hiyo ambapo kiingilio cha juu zaidi kitakuwa ni shilingi 20.000 huku cha chini kikiwa ni shilingi 3,000.

Uongozi wa DEDEBIT jana jioni ulitangaza kikosi kamili kitakachotua Bongo kuwakabili watoto wajangwani ambacho ni

VIONGOZI
1.Aleka G/Egizabihere Abreha…Kiongozi wa Msafala
2.G/Medhin Haile…….Kocha Mkuu
3.Zelalem Shiferawu…..Kocha Msaidizi
4. TsegaZeabe Asegedom…..Kocha wa makipa
5.Tibebe Aleme….......Meneja wa Timu