Tuesday, January 18, 2011

YANGA,ATLECTICO TAIFA LEO

Mabingwa wa zamani wa ligi kuu Tanzania bara Yanga leo wanataraji kujitupa uwanjani kupambana na mabingwa wa zamani wa brazil Atlectico fc katika uwanja mkuu wa taifa katika mchezo wa kimataifa wa kujipima nguvu.

Mchezo huo umeandaliwa na kampuni ya simu za mikononi ya vodacom kwa kushirikiana na cluods media group una lengo la kuvijaribu vikosi vya simba na yanga ambazo zote zinajiandaa kwa michuano ya kimataifa.
Akizungumzia pambano hilo afisa habari wa yanga luis sendeu amesema kuwa wao wamejiandaa vizuri kwa mtanange hiuo na kikosi kamili kipo tayari kuwakabili mabingwa hao wa zamani wa Brazil.

                                                                                          KIKOSI CHA YANGA
Timu ya Atlectico iliwasili juzi mchana na ikiwa hapa inatarajiwa kucheza mechi tatu za kirafiki zingine ni dhidi ya simba sc siku ya alhamisi,pia dhidi ya Azam fc siku ya jumamosi.