Monday, January 17, 2011

YANGA YACHOMOA KWA ZESCO

Timu ya soka ya yanga ya jijini jana iliingia mitini kwa kushindwa kujitokeza katika dimba la uhuru kucheza na mabingwa wa zambia ZESCO.

Mabingwa hao wa zambia wapo nchini kwa ziara ya timu za simba na yanga ambapo siku ya jumamosi walicheza na simba na kuitandika mabao 2-1.

Kwa mujibu wa taarifa zalizopatikana kutoka ndani ya klabu ya yanga zinasema kuwa yanga wameshindwa kupeleka timu uwanjani kwa shinikizo la kocha wao papic aliyeshauri ni bora timu ikaendelea na mazoezi ya kawaida.