![]() |
Dogo janja ndani ya Unifomu. |
Dogo janja ambaye sasa anatamba na ngoma yake mpya ya 'mtoto wa uswazi' aliyomshirikisha mkali toka salasala 'Godzilla' amesema kuwa atahakikisha matokeo ya midterm hii yanakua mazuri zaidi ili kuwatoa wasiwasi wazazi wake.
"Unajua kwa sasa nataka kupiga book mpaka nifanye vizuri ili wazazi wasiwe na wasiwasi kuwa muziki utanirudisha nyuma kielimu"alisema Dogo Janja.
Dogo janja anasema anaushukuru sana uongozi na wanafunzi wenzake wote wa Makongo High School kwa sababu wamempokea vizuri na anashirikiana nao vizuri katika masuala ya elimu.
![]() |
DOGO JANJARO. |