![]() |
Kikosi cha 'STARS' |
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo wanaingia dimbani katika dimba jipya la Taifa kukabiliana na 'vibonde'Timu ya Taifa ya Palestina katika mchezo maalum wa kirafiki uliopo katika kalenda inayotambuliwa na shirikisho la soka duniani FIFA
Stars inaingia uwanjani jioni ya leo pasipo nyota wake kadhaa kutoka kwenye timu za YANGA na MTIBWA SUGAR ambazo zilikuwa nje ya DAR ES SALAAM kwenye michuano ya ligi kuu Tanzania Bara mwishoni mwa wiki.
Kwa mujibu wa Afisa habari wa shirikisho la soka Tanzania TFF Boniface Wambura maandalizi kwa ajili ya pambano hilo yamekwisha kamilika na kinachosubiliwa ni muda mwafaka wa mtifuano huo.