![]() | ||
Kikosi cha Yanga |
Timu ya soka ya Yanga ys jijini Dar es Salaam jana waliianza vizuri ngwe ya pili ya ligi kuu ya soka Tanzania Bara maarufu kama Vodacom premier league baada ya kuichabanga bila huruma timu ya AFC ya Arusha mabao 6-1 mchezo uliofanyika kwenye dimba la uhuru.
Mashujaa wa yanga katika mtanange huo walikuwa ni Davis Mwape aliyetupia matatu wavuni,Iddi mbaga alifuga mawili pamoja na Shedrack Nsajigwa aliyefunga bao moja.